Idadi ya watu waliofariki kufuatia mkasa wa kuporomoka kwa jengo mtaani Huruma imeongezeka hadi 51.

Share news tips with us here at Hivisasa

Hii ni baada ya watu wawili kupoteza maisha yao wakati wakipokea matibabu katika hospitali kuu ya Kenyatta.

Juhudi za kutafuta manusura zaidi zikielekezwa katika mto wa Nairobi ulioko kandokando mwa jengo hilo.

Kwa sas, watu 28 hawajulikani waliko huku wengine 11 wakiendelea kupokea matibabu katika hospitali kuu ya Kenyatta.

Aidha, inakiziwa kuwa huenda watu zaidi walibebwa na maji walipokuwa wakijaribu kuhepa wakati wa kuporomoka kwa jengo hilo.