Share news tips with us here at Hivisasa

Idadi ya wagonjwa wanaougua ugonjwa wa kipindupindu katika Hospitali kuu ya Mogotio imeripotiwa kupungua kutoka wagonjwa 11 hadi sita.

Haya yamedhibitishwa na Afisa mkuu wa afya ya umma kwenye Kaunti ya Nakuru Samwel King'ori, aliyekuwa akizungumza na mwandishi huyu kupitia kwa njia ya simu siku ya Alhamisi.

King’ori alisema kwamba wagonjwa wasita ndio ambao wamelazwa kwenye hospitali hiyo kwa sasa.

Hata hivyo, alisema kwamba wagonjwa watano walitibiwa siku ya Jumatatu usiku na wakaruhusiwa kwenda nyumbani asubuhi ya Jumatano.

“Wagonjwa hao wametoka kwenye kaunti ndogo ya Rongai na Kaunti ya Baringo eneo la Mogotio,” alisema King’ori.

Mkurugenzi wa afya ya umma na usafi wa mazingira Dkt Joseph Lenai akizungumza wakati wa sherehe za kuadhimisha siku ya unawaji mikono duniani, alisema kwamba mkurupuko wa maradhi ya kipindupindu mjini Rongai umethibitiwa.