Idara ya Afya katika Kaunti ya Mombasa imesema kuwa itaanza zoezi ya kutathmini vyeti vya wahudumu wote katika sekta ya afya, haswa vya madikatari na wauguzi.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Akiongea afisini mwake siku ya Jumatatu, mkuu wa Idara ya Afya Mohammed Abdi alisema kuwa kuna haja ya vyeti hivyo kuangaliwa ili kuwafurusha madaktari na wauguzi bandia ambao wamekuwa wakiwahadaa wakaazi wa kaunti hiyo.

Aidha, Abdi alitoa wito kwa wananchi kutoa taarifa kwa maafisa wa afya iwapo wanashauku kuhusu mtu yeyote ama kituo chochote kinachotumika kama kliniki.

Idara hiyo pia ilitoa ripoti hivi majuzi inayo onyesha kuwa watu wengi hupoteza maisha kwa kupewa matibabu yasiyofaa katika kaunti hiyo.