Idara ya afya katika Kaunti ya Mombasa imeanzisha zoezi la kufunga kampuni zinazotengeneza maji ya chupa al maarufu 'mineral water' ambazo hazina leseni.

Share news tips with us here at Hivisasa

Akiongea baada ya kutekeleza oparesheni katika kampuni moja ya Zahara Water siku ya Ijumaa, mkuu wa Idara ya Afya katika Kaunti ya Mombasa Mohamed Abdi, alisema kuwa idara hiyo iliamua kufunga kampuni hizo baada ya maji wanazotengeneza kufanyiwa uchunguzi na kupatikana kuwa haifai kutumiwa na binadamu.

“Ningependa kuwatahadharisha wakaazi wa Mombasa kujiepusha na kutumia maji kutoka kwa kampuni kama Star Pop, Blue Wave na Zahara,” alisema Bwana Abdi.

Haya yanajiri baada ya kutokea mkurupuko wa ugonjwa wa homanyongo A katika kaunti hiyo, hali iliyosemekana kutokana na wakaazi kunywa maji machafu.