Idara ya jeshi nchini imekata rufaa kupinga kuachiliwa huru kwa wanajeshi 25 walioasi jeshi mwaka wa 2011.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

KDF, kupitia kwa mwendesha mashtaka wa jeshi, Brigedia Kenneth Dindi, imesema mahakama kuu ilikiuka sheria za jeshi ilipowaachilia huru wanajeshi hao.

Brigedia Dindi alisema wanajeshi zaidi ya 800 wameacha kazi tangu KDF kuingia Somalia.

Dindi aliongeza kuwa wanajeshi hao wameasi jeshi kwa masilahi yao binafsi na kujiunga na majeshi ya Marekani.

Mnamo Agosti 21, mwaka jana, Mahakama kuu ya Mombasa iliwaachilia huru wanajeshi 25 walioasi idara ya jeshi la wanamaji nchini katika kambi ya Mtongwe jijini Mombasa.

Wanajeshi hao walikuwa wamehukumiwa maisha na mahakama ya jeshi baada ya kupatikana na hatia ya kuasi jeshi.

Brigedia Dindi alisema Jaji Martin Muya hakuzingatia sheria wakati wa uamuzi wake.

KDF imesema kuwa hatua ya kuachiliwa huru kwa wanajeshi hao itawafanya wanajeshi zaidi kuasi idara ya jeshi nchini.