Wahanga wa ghasia za baada ya uchaguzi wa mwaka 2007 wamewataka wanasiasa kukoma kutoa semi zinazoleta chuki baina ya wakenya.
Wakikutana mjini Naivasha Jumatatu, wahanga hao walisema kuwa ni jambo la kusikitisha kuona mikutano inayofanywa ya kuonyesha hakuna imani na mashirika ya kiserikali na kuwaomba wakome.
Kulingana na Esther Namulanda: "Semi za muungano wa upinzani CORD kutaka kubanduliwa kwa IEBC hazifai na ningependa viongozi hao kuzingatia sheria kulingana na katiba."
Naye Mary Wandia aliyeadhiriwa wakati wa mkasa wa kanisa la Kiambaa amesema kuwa "Katu hatungetaka kuona yale yaliyotendeka wakati wa ghasia za 2007-08 kutendeka hivi sasa, na nawaomba wakenya kuishi pamoja kwa amani.