Wahanga wa machafuko ya baada ya uchaguzi huko Njoro wamepongeza hatua na kusitishwa kwa kesi ya naibu rais William Ruto na mwanahabari Joshua Sang huku wakijivunia kuwa Mola amejibu dua yao.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Wakizungumza mwanahabari huyu Jumatano, maafisa wa wahanga hao zaidi ya 6,400 wamemtaka naibu rais Ruto kutimiza ahadi yake kuwa, sasa ataongoza shughuli za kuwapa makao idps waliosalia kushughulikiwa.Wamemtaka mbunge wao Joseph Kiuna kujitolea kuwashughulikia pamoja na kuwaunga mkono.

Mwenyekiti wao David Temberewa ameitaka serikali kuwapa mashamba yaliyotambuliwa ili kuendesha maisha yao kikawaida kama lile la Githima huko Njoro, Kitingel na la Tipis.

"Tunataka pia walionyakua mashamba na maploti katika eneo la Kabiemet na Milimani Njoro kuyarejeshea wenyewe" Temberewa aliongeza.

Akiandamana na wenzake Elijah Okwema ambaye ni mweka hazina wa wahanga hao na mwanachama Austine Sang, viongozi hao wametaka mizozo ya mashamba katika jimbo hili kama vile Ngongongeri huko Njoro na Ndabibi Naivasha kutatauliwa kabisa ili kutapatikane amani kamili.

Kuhusi vijana wa huduma kwa taifa NYS waliokamilisha mafunzo yao zaidi ya mwaka mmoja uliopita, wameitaka serikali kuwapa nafasi ya kwanza katika uajiri wa maafisa wa idara za usalama. Idps hao wanatoka jamii 8 za hapa nchini.