Tume Huru ya Uchaguzi na Uratibu wa Mipaka Nchini (IEBC) imesema kuwa uchunguzi utafanywa ili kubaini kilichosababisha idadi kubwa ya wapiga kura kuhamia vituo vipya vya kujisajili kama wapiga kura.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Kwenye ripoti yake ya mwisho kuhusu zoezi la kuwasajili wapiga kura lililokamilika tarehe 15, mwezi huu, IEBC ilikiri kuwa hali hiyo ya wapiga kura kuhama ilishuhudiwa pakubwa na haikuwa ya kawaida.

‘‘Kiini cha watu kuhamia vituo vipya vya uchaguzi kinahitaji kuchunguzwa na kuchanganuliwa kwa kina kwani ni suala ambalo haliwezi tupiliwa mbali kwa kuhusishwa moja kwa moja na uhamiaji wa watu kwa makaazi mapya,’’ alisema mwenyekiti wa IEBC, Isaack Hassan.

Kulingana na takwimu zilizotolewa na tume ya IEBC, takriban wapiga kura 493,169 walihama kutoka vituo vyao vya zamani vya kupigia kura na kuenda kujisajili katika vituo vingine katika wadi, maeneo bunge na hata kaunti.

Hassan alisema kuwa kuwa hali hiyo ya wapiga kura kuhama ilishuhudiwa katika kaunti zote 47.