Mwanasiasa na mchanganuzi wa maswala ya kisiasa Koigi wa Wamwere amesema ni lazima tume huru ya mipaka na uchaguzi IEBC iondoke afisini kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2017
Akizungumza hii leo,Koigi amesema tume ya uchaguzi lazima ivunjwe iwapo serikali ina nia ya kuleta amani kabla na baada ya uchaguzi.
“Serikali inapaswa kuishinikiza IEBC kujiuluzu kama vile ilivyolazimisha baraza la mitihani kujiuzulu baada ya kuhusishwa na ufisadi na kampuni ya Smith and Ouzman.IEBC imekatiliwa kitaifa na hata kimataifa na sioni ni kwa nini serikali inaendelea kutetea tume ambayo imezongwa na ufisadi," akasema koigi
Koigi alitoa mfano wa mahakama ambapo jaji hawezi kuendela kusikiza kesi ambayo mlalamishi hamtaki
"Kama upadne mmoja wa kesi umetoa tetesi kuhusu jaji anayesikiza kesi basi itamlazimu jaji huyo ajiondoe katika kesi hiyo na IEBC inapaswa kufanya hivyo," Koigi alisema.
Koigi hata hivyo aliwataka wakenya kujiepusha na vurugu wakati wanapoandaa maandamano ya kuitaka IEBC kungatuka.