Tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC, imetoa utaratibu wa jinsi inavyolenga kutumia shilingi bilioni 19 kutoka kwa Wizara ya Fedha kufadhili uchaguzi mkuu wa 2017.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Afisa mkuu mtendaji wa Tume ya IEBC, Ezra Chiloba, aliiambia kamati ya bunge kuhusu sheria kuwa wanatazamia kutumia shilingi bilioni 4.4 kuwaajiri maafisa wa kuvisiamamia vituo vya kupigia kura na shilingi bilioni 2.7 kwa usafirishaji wa vifaa vya kupigia kura.

Chiloba vilevile alieleza kuwa tume hiyo inalenga kutumia shilingi bilioni 3.2 kwa awamu ya pili ya usajili wa wapiga kura itakayofanyika kuanzia mwezi Februari hadi Machi 2017.

Akizungumza siku ya Alhamisi walipofika mbele ya kamati ya bunge kuhusu sheria, Kamishna wa IEBC Mohammed Alawi alisema kuwa iwapo ombi lao la fedha hizo litapitishwa, wataweza kuagiza vifaa vya kura mapema ili vijaribiwe mapema.

"Vifaa hivyo vitafika nchini mwezi Machi mwaka ujao," alisema Alawi.