Afisa mkuu wa idara ya usajili wa watu kanda ya Pwani Aggrey Masai, amepinga madai yaliyotolewa na tume ya uchaguzi na uratibu wa mipaka nchini IEBC kuwa idadi ndogo ya watu waliyojisajili kuwa wapiga kura imetokana na idara hiyo kutoa vitambulisho kidogo.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Akizungumza mjini Mombasa siku ya Jumatano, Masai amesema kuwa idara hiyo kanda ya Pwani imekuwa ikitoa vitambulisho kwa Wapwani wengi kila mwaka ila wakaazi wenyewe ndio hawajajitokeza kwa usajili huo kutokana na ukosefu wa hamasa.

Masai amesema kuwa tume ya IEBC inafaa kuwahamasisha Wapwani na Wakenya kwa jumla kuhusu umuhimu wa usajili wa wapiga kura ili kufikia malengo yao ya kupata zaidi ya Wakenya milioni 18.

"IEBC haipaswi kutulaumu kuwa kuandisha idadi ndogo ya wasajili wa wapiga kura kufuatia madai kuwa tumetoa vitambulisho kidogo kwa wakenya, liso sio swala la kujadili tume hiyo inafaa kupenya hamasa kwa wananchi kuhusu usajili wa wapiga kura," alisema Masai.

Awamu ya kwanza ya zoezi la usajili wa wapiga kura lilikamika siku ya Jumanne kote nchini huku tume hiyo akisema kuwa kamwe haitaongeza muda zaidi wa zoezi hilo hadi mwaka ujao mwezi Februari.