Utendakazi wa tume ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC unaendelea kukosolewa.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Mbunge wa Westalands,Tim Wanyonyi katika mahojiano ya moja kwa moja na kituo cha redio cha Citizen siku ya Jumatano katika kipindi cha Jambo, alisema kuwa utendakazi wa tume hiyo ni duni na hawana budi kuondoka ofisini huku ikizingatiwa kuwa chama cha Cord kiliapa kufanya maandamano kila Jumatatu kushinikiza tume hiyo kutimuliwa ofisini.

Wanyonyi aliongezea kuwa Cord kimemwandikia barua Rais Kenyatta kumtaka awaarike kwa majadiliano ya kuwaondoa makamishna wa IEBC ofisini. Hii ni baada ya mashirika mbalimbali nchini kuunga mkono kuondolewa kwa makamishna wa IEBC ofisini kwa kuwa wamehusishwa na ufisadi na ikidaiwa kuwa hawana uwezo wa kusimamia uchaguzi mkuu ujao.