Licha ya maafisa wa polisi kukamata misokoto ya bangi 1400 katika mji mkuu wa kitalii katika eneo la Pwani huko Mtwapa kaunti ndogo ya Kilifi Kusini imezua hisia mseto baina ya wakaazi eneo la Pwani.
Wakaazi wa Pwani wameachwa na maswali mengi bila majibu ni vipi bangi hiyo iliweza kupita vizuizi vyote vya polisi kutoka kwa mpaka wa nchi ya Kenya na Tanzania.
Wamezidi kusema kuwa kuna uzembe ambao unaweza kushudiwa katika idara ya polisi nchini na hali hiyo inastahili kukabiliwa ipasavyo.
Kwa mujibu wa afisaa mkuu wa upelelezi wa kaunti ya Kilifi Jason Mworia, maafisa wa polisi walipashwa habari kabla ya kuvamia nyumba iliyokuwa hifadhi ya bangi hiyo huko Mtwapa.
Wakati wa oparesheni hiyo polisi walifanikiwa kuwatia mbaroni washukiwa wawili ambao ni Samuel Oduor na Nickson Oduor ambao kwa sasa wanazuiliwa katika kituo cha polisi cha Mtwapa wakisubiri kufikishwa mahakamani.
Aidha wakaazi hao wamesema kuwa kuwatia mbaroni watu hawa sio suluhisho ila swali ni kuwa ni ni vipi bangi hiyo iliweza kufika mtwapa na kunawalinda usalama kwenye barabara.
Hata hivyo serekali imetakiwa kuingilia kati na kupiga vita swala hilo la mihadarati kwenye eneo la Pwani.