Inspekta wa polisi nchini Joseph Boinett ameombwa kuingilia kati kisa kilichotendeka Kisii na kutuma maafisa wa polisi katika kituo cha polisi cha Kenyenya eneo bunge la Bomachoge Borabu kufanya uchunguzi na kuwatia mbaroni washukiwa waliomkata mkono jirani yao katika eneo la Kenyenya.

Share news tips with us here at Hivisasa

Wito huo umetolewa baada ya Patrick Obare kukatwa mikono yake kwa miezi minane iliyopita na majirani wake huku maafisa wa polisi wa kituo hicho wakiahidi kufanya uchunguzi kuhusiana na kisa hicho jambo ambalo halijashughulikiwa hadi sasa .

Akizungumza nasi, mmoja wa watetezi wa haki za binadamu katika kaunti ya kisii Tom Osoro alimwomba Boinett kutuma maafisa wa polisi kufanya uchunguzi huo ili haki kutendeka kwa aliyekatwa mikono ambaye hawezi fanya kazi ili kulisha familia yake.

“Maafisa wa polisi wa Kenyenya waliahidi kufanya uchunguzi na kuwatia mbaroni washukiwa waliomkata jirani yao mkono, lakini hadi sasa wanatembea wakiwa na huru, hakuna hatua iliyochukuliwa dhidi yao,” alisema Osoro.