Eneo la kutupa taka la mji wa Naivasha linaongoza kwenye uharibifu wa mazingira ikiwemo ziwa la Naivasha.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Tukio hilo limeifanya serikali ya kaunti ya Nakuru kukarabati sehemu hiyo iliyoko eneo la Kayole, yapata kilomita tatu kutoka mji wa Naivasha.

Aidha, mvua kubwa inayoendelea kunyesha imesababisha vifo vya samaki kwani taka hizo huwa na kemikali za sumu, ambazo huoshwa na kuingia kwenye ziwa hilo.

Mwenyekiti wa kamati ya utekelezaji wa bunge la Kaunti ya Nakuru Simon Wanango amesema sehemu hiyo pia itawekwa ua la kudumu, kama njia moja ya kuzingatia mazingira bora.

Akizungumza mjini Naivasha Alhamisi, Wanango amesema kuwa sehemu hiyo imekuwa ikihatarisha maisha ya wengi kiafya, kwani imejaa huku ikionekana kuwa juhudi za kununua sehemu mpya zimegonga mwamba.

“Uwanja huu umekuwa ukihatarisha maisha ya watu wengi kiafya kwa sababu umejaa taka,” alisema Wanango.