Mwakilishi wa Wadi ya Kongowea Jabez Oduor katika hafla ya awali. [Picha/ barakafm.org]Mwaniaji wa kiti cha useneta kupitia chama cha Wiper Jabez Odour amepoteza nafasi hiyo baada ya kushindwa na mpinzani wake Lawrence Kisilu kwenye kura ya mchujo.Odour, ambaye pia ni Mwakilishi wa Wadi ya Kongowea alipata kura 3,409 huku Lawrence Kisilu akipata kura 4,078.Hatua hii inaonekana kuwa pigo kwa Jabez, ikizingatiwa amepoteza nafasi hiyo pamoja na ile ya uwakilishi wadi.Vile vile, Jabez anakabiliwa na kesi ya kuzua fujo wakati wa kura hizo za mchujo siku ya Jumanne katika Shule ya msingi ya Fahari huko Kiziwi.Jabez aidha alikabiliwa na shtaka la pili la kuzuia polisi kutekeleza majukumu yao kikatiba.Hata hivyo, alikanusha madai hayo mbele ya Hakimu Henry Nyakweba siku ya Jumatano.Hakimu Nyakweba alimuachilia kwa dhamana ya shilingi laki moja ama shilingi elfu 50 pesa taslimu.Kesi hiyo itatajwa Mei 8 mwaka huu.
MOMBASA
Jabez ashindwa kwenye kura za mchujo za useneta
ADVERTISEMENT
Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know
Thank you for reading my article! You have contributed to my success as a writer. The articles you choose to read on Hivisasa help shape the content we offer.
-Osman Suleiman