Gavana wa Mombasa Hassan Joho.[tuko.co.ke]

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Jaji Lydia Achode anayesikiliza kesi ya kupinga ushindi wa gavana wa Mombasa Hassan Joho amedinda kujiondoa kwenye kesi hiyo licha ya kutakiwa ajiondoe.

 Hii ni baada ya  aliyekuwa Seneta wa Mombasa Hassan Omar kuwasilisha ombi hilo kwa kudai kuwa hana imani na jaji huyo.

Sarai anadai kuwa Jaji Lydia Achonde wa Mahakama ya Mombasa anapendelea upande wa Joho na hatoi usawa katika kesi hiyo.

Akitoa uamuzi huo siku ya Jumatatu jaji Achode alilitaja ombi la Sarai kama lisilokuwa na msingi wowote wa manna wa kumfanya ajitondoe kwenye kesi hiyo.

Alisema kuwa hawezi kupendelea upande wa Joho na kusisitiza kuwa sheria na kanuni za idara ya mahakama hazimruhusu kupendelea upande wowote.

Achode alisema kuwa katiba inamruhusu kusikiliza kesi za uchaguzi hivyo hawezi kujiondoa kamwe.

Amemtaka Sarai kukata rufaa iwapo hajaridhika na uamuzi huo.

Siku ya Alhamisi wiki iliyopita seneta Omar Sarai kupitia wakili wake Yusuf Abubakar ametaka ombi hilo kusikilizwa kwa haraka ili kutoa fursa kwa Jaji mkuu David Maraga kuteua jaji mwengine kusikiliza kesi hiyo.

“Tunataka ombi letu kusikilizwa kwa haraka ili kutoa nafasi kwa Jaji mkuu kuteuwa jaji mwengine ambaye hana upendeleo wowote,” alisema Abubakar.

Abubabak amedai kuwa Jaji Achode amekuwa na upendeleo dhahiri kwa upande wa Gavana Joho na kusema kuwa hakuna haki na usawa utakaopatikana kwenye kesi hiyo iwapo jaji huyo ataendelea kuisikiliza.

“Tunaohofia kuwa mteja wangu hatapata haki na uamuzi wa usawa kwa sababu kuna upendeleo fulani unaendelea kwenye kesi hii,” alisema Abubakar.

Omar aliwasilisha kesi hiyo mahakamani kupinga ushindi wa Gavana Joho kwa madai kuwa uchaguzi wa Agosti 8 haukuwa wa huru na wazi.

Tayari zaidi ya mashahidi 20 wametoa ushahidi wao kwenye kesi hiyo.

Mashahidi wengine wanatarajiwa kuendelea kutoa ushahidi wao 24,1,2018.