Jaji mmoja katika mahakama ya Keroka kwa jina Christus Nambabu ameshtakiwa kwa afisi ya watoto iliyoko eneo la Borabu kaunti ya Nyamira kwa kunyanyapa maslahi ya mwanawe aliyezaa na afisa wa polisi katika kitengo cha utawala.

Share news tips with us here at Hivisasa

Kulingana na afisa huyo wa utawala kwa jina Grace Wangoi, Jaji huyo alianza kuwa na mapenzi naye mwaka 2014 huku wakifanikiwa mtoto ambaye sasa jaji huyo amekataa kuchukua majukumu ya uzazi na kumwachia afisa huyo kutekeleza majukumu hayo pekee yake jambo ambalo lilimlazimisha kufika kwa afisi ya watoto na kumshtaki.

Akizungumza siku ya Alhamisi katika afisi hiyo ya watoto, Wangoi alisema alimshtaki jaji huyo ili kufika kwa afisi hiyo kueleza kwa nini hataki kuchukua majukumu ya mzazi na kumwachia pekee yake.

“Mimi nilianza kuwa na mapenzi na jaji huyo ambaye anafanya katika mahakama ya Keroka ninataka naye awe anachukua majukumu haya kama mzazi badala ya kuniachia mimi mweyewe,” alisema Wangoi.

Aidha, afisa anayeshughulikia mambo hayo katika afisi ya watoto kwa jina Martha Mbatia alimwandikia barua jaji huyo kufika mbele ya afisi hiyo ili kueleza chanzo cha kujitenga na majukumu ya uzazi.