Gavana wa kaunti ya Garissa Nadhif Jama alilazwa katika hospitali ya Aga Khan mjini Kisumu akiuguza majeraha.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Gavana huyo inasemekana kuwa aliteguka akishuka kutoka katika ndege, jambo lilipelekea kuanguka na kupata majeraha.

Jama alikuwa akiwasili katika kaunti ya Kisumu tayari kuhudhuria kongamano la magavana kuhusu ugatuzi linalo lilioanza hiyo jana.

Kongamano hilo lilifunguliwa rasmi na raisi Uhuru Kenyatta, ambaye yuko katika ziara mkoa wa Nyanza.

Kiini cha hafla hiyo ni kutathmini mafanikio na matunda ya serikali za ugatuzi tangu zichukue hatamu za uongozi.

Wageni mashuhuri kutoka sehemu mbalimbali hapa nchini pia wanahudhuria zoezi hilo, huku usalama ukiwa umeimarishwa ili kuhakikisha shughuli hiyo inaendelea bila bughudha yoyote.

Kongamano hilo ni la pili, baada ya la kwanza kufanyika katika kaunti ya Kwale ambalo lilishuhudia magavana wote 47 wakihudhuria.

Kokangamano hilo liling’oa nanga bila tashwishwi yeyote, na linaingia siku ya pili hii leo.