Mwanaume mmoja mwenye umri wa makamo kwa jina Livingstone Wepukhulu amefikishwa mbele ya hakimu mkuu Benard Mararo katika mahakama ya Nakuru Jumatano na kushtakiwa kwa kosa la kumnajisi mwanamke anayedaiwa kuwa mwenye akili taahira.
Inadaiwa kuwa, tarehe Mei 12 katika eneo la Naka kaunti ya Nakuru, mshukiwa alimvamia mwathiriwa na kumfanyia unyama huo..
Mshukiwa alikanusha mastaka hayo na kuachiliwa kwa bodi ya shilingi 200, 000 na mdhamini mmoja wa kiwango sawa na hicho huku kesi hiyo ikiratibiwa kutajwa tarehe Juni 6 na kusikilizwa tarehe kumi na moja mwezi wa julai mwaka huu.