Mwanamme mmoja kwa jina la Shadrack Kibet mwenye umri wa makamo amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu gerezani kwa wizi wa simu yenye thamani ya shilingi elfu kumi katika mahakama moja ya Nakuru.
Mshukiwa alipatilizwa kifungo hicho Jumatano.
Kibet alishtakiwa kwa kosa la kumwibia msichana mmoja kwa jina la Beatrice Wanjiku simu yake akiwa katika mahakama ya Nakuru.
Mshukiwa huyo anadaiwa kunyemelea mkoba wa Beatrice Wanjiku bila yeye kujua na akapora simu yake ya mkononi.
Punde tu msichana huyo kugundua kwamba simu yake haipo tena ilimbidi awajulishe maafisa wa polisi katika mahakama hiyo.
Mshukiwa alionekana akiwa na wasiwasi mwingi.
Kiongozi wa mashtaka aliamuru maafisa wa polisi kumchunguza mshukiwa na hatimaye alipatikana na simu hiyo.
Mwanumme huyo alikiri madai hayo mbele ya hakimu mkuu David Kemei.