Kioja kilitokea Jumapili katika eneo la Mzee Wanyama Pipeline, baada ya jamaa mmoja kufumaniwa akila uroda na mke wa wenyewe.
Jamaa huyo alifumaniwa akijivinjari utamu wa barafu ya jirani yake katika shamba moja la ndizi, na kupewa kichapo cha mbwa katika kisa hicho cha mchana jua likichoma kitosini.
Wakaazi waliokuwa na hasira chungu nzima, waliwalazimisha wawili hao kutoa nguo na kuendelea kula uroda mbele yao huku nao Wakenya wabunifu, watumizi wa mitandao, wakichukua fursa hiyo kuweka matokeo yote kwenye rekodi za video.
Kulingana na shahidi mmoja kwa jina Geofrey Wanyonyi, mume wa mwanamke huyo hakuwa karibu wakati wa kisanga hicho.
“Katika jamii yetu ni vibaya sana kwa mtu kujamiana na mke wa wenyewe na ilikuwa ni bahati tu wakapatikana kwa sababu mumewe huja jioni kutoka kazini. Unaweza hata kurogwa,” alisema Wanyonyi.