Maafisa wa polisi katika kituo cha Ferry wanamzuilia mwanamume mmoja aliyejirusha baharini akiwa na lengo la kujiuwa.

Share news tips with us here at Hivisasa

Benson Njau ametiwa mbaroni baada ya kuokolewa na maafisa wa uogoleaji muda mfupi tu baada ya kujirusha majini kutoka kwa ferry ya Mv. Nyayo.

Mkuu wa polisi eneo la Likoni Willy Simba amesema kuwa si mara ya kwanza kwa mwanamume huyo kutaka kujiuwa kwa kujirusha baharini, na kwamba mwishoni mwa mwezi wa tano pia alitaka kujiua na alifikishwa mahakamani ambapo aliwachiliwa kwa masharti.

“Si mara ya kwanza kwa jamaa huyu kutekeleza kisa kama hiki. Mwezi Mei pia alijirusha majini na kufikishwa mahakani kisha akaachiliwa,” Simba alisema.

Njau sasa anatarajiwa kufikishwa mahakamani juma hili.