Watu watatu wamefikishwa kizimbani na kufunguliwa mashtaka ya ulaghai wa shilingi milioni 4.4.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Mnamo Januari 12, 2015, Moses Karigo, Eunice Nyambura na Dickson Kimani wanadaiwa kumlaghai shilingi milioni 4.4 mfanyibiashara Antony Murith kwa lengo la kumuuzia magunia elfu mbili ya mchele.

Watatu hao walidanganya kuwa wangeweza kusambaza mchele huo hadi katika duka jumla la Tuskeys iliyoko eneo la Shimanzi.

Siku ya Ijumaa, wote wamekanusha mashtaka hayo mbele ya hakimu Irene Ruguru.

Kesi hiyo itatajwa Julai 6,2016 ilikuchanganywa na kesi sawia na hiyo.