Jamii ya Pwani imehimizwa kutowabagua walemavu na badala yake kuwashirikisha katika shughuli mbalimbali pamoja na watu wengine wasiyokuwa na changamoto za kimaumbile.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Afisia Mkuu wa Shirika la Msalaba mwekundu katika kaunti ya Mombasa Mohammed Rajab Said amesema kwamba walemavu wamekuwa wakibaguliwa hali inayowasababishia changamoto nyingi maishani na akaitaka jamii ya Pwani kuwathamini walemavu.

Akizungumza mjini Mombasa siku ya Ijumaa katika mkutano wa maandalizi ya sherehe inayowahusisha Watoto walemavu ili kukumbuka mwanzilishi wa Shirika la Msalaba mwekundu Henry Dunat itakayofanyika tarehe 29 mwezi huu Mjini Mombasa, Rajab amesema kwamba sherehe hiyo imewalenga Watoto walemavu ili kuwaondoela upweke na kutengwa.

"Tunapanga maandalizi hayo ili kuhakikisha kuwa tunawaondolewa watoto walemavu upweke na kuwashirikisha vyema na jamii zao na wakaazi ili kuona kwamba walemavu pia wanatambulika",alisema Rajab.

Akisema kwamba Shirika hilo linahitaji ufadhili wa vyakula na zawadi kwa watoto hao, mhudumu huyo wa kibinadamu mjini Mombasa amewasihi wahisani kujitolea na kuwasilisha misada yao ya vyakula na bidhaa zozote za kibinadamu katika afisi za Shirika hilo mjini Mombasa.