Rais Uhuru Kenyatta akiwa na wanadensi kutoka jamii ya Mijikenda eneo la Shika Adabu. [Picha/Standard]

Share news tips with us here at Hivisasa

Baadhi ya wanasiasa kutoka pwani ya Kenya wamemlaumu rais Uhuru Kenyatta kwa kuibagua jamii ya Mijikenda wakati alipoteua baraza lake la Mawaziri.

Mbunge wa Kilifi Kaskazini Owen Baya, Paul Katana (Kaloleni), Teddy Mwambire (Ganze) Michael Kingi (Magarini) na aliyekuwa mbunge wa Bahari John Mumba wanasema kuwa rais angemteua hata ntuu mmoja kutoka jamii hiyo.

Owen Baya alisema kuwa hatua hiyo inaonyesha kuwa Hatua hiyo inaonyesha wazi kuwa rais Kenyatta haijali jamii ya Mijikenda.

“Hii ni kinyume na sheria ambapo inasema wazi kuwa mawaziri wanahitaji kuteuliwa kutoka kila sehemu nchini,” Alisema Baya.

Naye Mbunge wa Kaloleni Paul Katana alisenma kuwa jamii ya Mijikenda inahitaji kuunga mkono muungano wa NASA kutokana na hatua hiyo.

Kwa upande wake mbunge wa Magarini Michael Kingi alisema kuwa baraza jipya la mawaziri linakosa sura ya taifa.

“Ikiwa tutazungumzia serikali kwa mtazamo wa kitaifa, basi jamii yetu ya Mijikenda ingejumuishwa,” alisema Kingi.

Mathias Keah, Katana Ngala, Gonzi Rai na Kassim Mwamzandi ni baadhi ya wakenya kutoka jamii ya Mijikenda ambao walihudumu kama Mawaziri  na manaibu mawaziri katika serikali ya rais mstaafu Daniel Moi.