Viongozi kutoka jamii ya Ogiek wameipongeza serikali ya jimbo la Nakuru, hasaa bunge lake, kwa kile walidai kuwa kuwahusisha katika hatua za kufanikisha maendeleo ya jimbo.
Wakiongea Mjini Nakuru kupitia kwa aliyekuwa mwakilishi wa Wadi ya Kuresoi kusini David Sitienei, wanajamii hiyo wamesema kuwa kwa mara nyingi, jamii yao hudunishwa ama hukosa kuhusishwa katika maswala mengi nchini, huku akiipongeza serikali ya gavana Kinuthia Mbugua kwa kuwaonyesha usawa na jamii zingine.
Amedokeza kuwa hatua hii ni kufuatia mmoja wao kuteuliwa katika bodi iliyoteuliwa maajuzi na itakayoshughulika maswala ya mashamba katika jimbo.
Hata hivyo, wametoa ujumbe kwa gavana kuwa ipo haja kuzingatia kuwa jamii zote zinawakilishwa hasaa wakati wa kupeana ajira za jimbo, akihoji kuwa jimbo hilo litaimarika tu iwapo jamii zote zitapewa nafasi za kuchangia kwa vyovyote vile na kwa usawa.
Kuhusu swala la upendeleo wa jamii mbili katika uteuzi wa maajuzi katika bodi husika, Sietinei amepuzilia mbali madai hayo kwa misingi kuwa jamii ya Kalenjini iko na kabila nyingi chini yake, huku akiongeza kuwa walioteuliwa ni wale wale waliofikia matakwa ya zoezi husika.
Itakumbukwa kuwa jamii ya Ogiek inatambulika kuwa jamii ya wachache na ambao hujihusisha na ufugaji wa nyuki sawia na maswala ya msituni.