Usalama umeimarishwa kwenye barabara kuu ya Mai Mahiu kuelekea Narok kufuatia ripoti kuwa jamii ya wafugaji inanunia kuifunga kutokana na mradi unaoendelea wa reli yakisasa ya SGR.

Share news tips with us here at Hivisasa

Jamii hiyo ya wamaasai inalalamikia kutonufaika na maendeleo ya miradi ya mvuke na reli hiyo inayofanyika eneo hilo.

Wakizungumza na wanahabari mapema Jumatano, mmoja wa wakaazi hao Joseph Salash alidai kwa kusema; “Ardhi ambayo miradi hii miwili inaendelezwa ni ya mababu zetu na tunafaa kuangaliwa ili hata sisi tunufaike.”

Haya yamejiri huku vijana wa eneo la Naivasha wakifanya mkutano kwa mara ya pili ili kuweza kuona jinsi ya kuwachagua viongozi watakaowaakilisha kwenye miradi hiyo ili kuwe na usawa.

Kiongozi mmoja wa vijana, Mwangi Muraya alisema; “Hatutasimama na kuona miradi hii ikifanyika bila ya sisi kuhusishwa ili wote tuweze kupata nafasi za kazi.”