Mgombea ujumbe wa Mogirango Magharibi wakili Steven Mogaka ameiomba jamii ya mkisii kuwa pamoja mwakani ili wawe na usemi katika serikari ijayo.
Akiwarai wakazi wa Mogirango Magharibi kwake siku ya Jumapili, wakili huyo aliwaomba wenyeji kuungana na kuwa fungu moja ili nao wawe wakusema ila si wa kupitiwa tu.
"Naomba ndugu zangu tuwe pamoja kwa amani ili tutakapofika uchaguzi ujao tuwe na serikali yenye tuna usemi wala si watu wa kupitiwa na kuhudhuriwa kwa barabara ama vituo vya magari," alisema Mogaka.
Hili linajili baada ya Rais Uhuru kuzuru kaunti ya Nyamira na kuhutubia wanainchi kando kando ya barabara kwa kuwa wanainchi wa Nyamira kuunga mkono muungano pinzani wa Cord.
Wakili huyo vile vile aliwahimiza wakazi hao kuwa na amani na upendo na kizidi kuwaombea viongozi wote bila kujali mrengo wao wa kisiasa.
Fauka ya hayo, wakili Mogaka alisema kwamba jamii ya mkisii imebaki nyuma sana kimaendeleo na nyadhifa mbali mbali za uongozi.
Mogaka ambaye amegombea kiti cha ubunge kwa mara mbili bila kufanikiwa bado amo uwanjani kuwania kiti hicho cha Mogirango magharibi ambacho kwa sasa kimewavutia wagombezi wengi wakiwa mawakili.