Watu wanaoishi na ulemavu katika eneo la Pwani watanufaika na ufadhili wa shilingi milioni 7.2 kutoka Serikali Kuu.

Share news tips with us here at Hivisasa

Mwenyekiti wa Hazina ya Taifa ya Watu Wanaoishi na Ulemavu Christine Kenyatta alisema walemavu wanastahili kuwezeshwa kibiashara ili waweze kujiendeleza maishani.

Akizungumza alipowakabidhi walemavu vifaa tofauti vya kazi katika makao makuu ya Ukanda wa Pwani mjini Mombasa, Kenyatta alisema kila Kaunti itanufaika na shilingi milioni 1.1, ambazoo walemavu watanunuliwa vifaa au kujengewa maeneo maalum ya kuendeleza kazi zao.

“Tumetoa ufadhili huu kuwasaidia walemavu nchini ili kuboresha maisha yao vyema hasa katika ununuzi wa vifaa vya matumizi na kujiendeleza katika biashara ndogo ndogo," alisema Christine.

Hatua hiyo imepokelewa vyema na wanaharakati wa kutetea haki za kibinadamu na jamii, wakisema kuwa hatua hiyo imewatambua vyema walemavu hasa eneo la Pwani.