Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Inasemekana kuwa madaktari wanaofanya kazi katika hospitali mbalimbali kwenye kaunti ya Garissa wanaendeleza ukeketaji kinyume na sheria za udaktari.

Wengi wa madaktari hao wanawapasha watoto wadogo, wenye umri wa mwaka mmoja hadi kumi na minne tohara. Ukeketaji unazidi kuendelezwa vijijini ambapo 75% ya wanaopashwa tohara wanapashwa kulingana na mila zao na akina mama vijijini. Wasichana wanaopashwa tohara hukumbana na changamoto nyingi sana.

Baadhi ya changamoto hizi ni;

• Kupata maumivu kwenye sehemu za siri nyakati za kufanya mapenzi na waume wao.

• Kutopata watoto wakiolewa. Sababu kuu ikiwa ni kutokuwa na uangalifu wakati wa kupashwa tohara.

• Kuona maumivu makali nyakati za kujifungua kwa watakaobahatika kufaulu kupashwa tohara vizuri.

Takwimu za hivi karibuni zinaonyesha kuwa jamii ya wasomali ndio inayoongoza ukeketaji kwa asilimia 36 wengi wao wakiwa wasichana wadogo. Wanawake wenye umri wa 15 hadi 25 kutoka jamii mbalimbali ndio wanaopashwa tohara kote mkoani kaskazini mashariki.

Haya yanajiri wakati mila ya ukeketaji iliyopitwa na wakati ikipigwa marufuku na kukemewa nchini, haswa kaunti ya Garissa.