Share news tips with us here at Hivisasa

Shirika linanalo toa huduma za bure kwa umma katika Kaunti ya Mombasa la 'Glad Organisation', limewaleta pamoja jamii zinazoishi mtaani katika uwanja wa Makadara na kuwaosha miguu, kama njia moja ya kukabiliana na funza ambao wamekuwa kero kubwa kwa jamii hiyo.

Akizungumza siku ya Jumamosi, mshirikishi wa shirika hilo Abdi Ali, ambaye ndiye alikuwa akiongoza huduma hiyo, alisema kuwa kivutio cha kuwapata watu hao ilikuwa kupitia michezo na baada ya hapo kuwapa chakula cha mchana.

Aliongeza kuwa vijana wengi walishuhudia hafla hiyo na kujitokeza kuangaliwa usafi wa miguu, ambapo waliweza kutolewa funza na kuwekwa dawa kwenye vidole ili funza wasiweze kuendelea kuharibu miguu yao.

Aidha, Ali alitoa wito kwa mashirika ya kiserekali pamoja na yale ya kibinafi kuangazia swala hilo na kukabiliana na tatizo la funza miongoni mwa jamii hiyo.

Aidha, mshirikishi huyo alisema kuwa watu hao wanahitaji msaada wa dharura kwa kupewa maakazi mbadala ili kuwaepusha na changamoto zinazowakumba.