Mnazi ni aina ya pombe ambayo wapwani wanaienzi.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Walakini, hivi karibuni kumekua na lawama zinazotokana na utumizi mbovu wa pombe ya mnazi.

Vijana kwa wazee wamekua wakibugia pombe hii kiholela.

Matokeo ni ya kuogofya. Familia zimevunjwa, masomo yakakatizwa, watu wamepigana na mengineyo.

Hili sio lengo kuu la mababu walioanzishi desturi ya kunywa tembo ya mnazi.

Wazee walitumia tembo hii kwa shughuli mbalimbali kama vile kueneza amani.

Utengamano ni muhimu sana katika jamii. Hili ni swala nyeti katika nchi yetu kwa sasa. Hutuambatani kama mbingu na ardhi.

Mababu walitumia wakati wa kunywa mnazi kuendeleza amani katika jamii. Waliwapa wasia wenzao kuhusu kulinda familia na kuishi pamoja.

Kuhifadhi utamaduni ni baadhi ya lengo kuu la kinywaji hiki.

Wazee walikitumia kupitisha utamaduni kutoka kizazi kimoja hadi kingine.

Maneno fulani yalielezwa kwa rika tofauti tofauti katika vikao ambavyo manzi uliandaliwa.

Katika sherehe kama vile za jando na unyago, mnazi hutumiwa kwa lengo kadhaa.

Wagema hutumia mvinyo kama kitega uchumi. Wao huuza pombe hii ili kuwatafutia wanao mlo, kuwanunulia mavazi pamoja na kuwalipia karo ya shule.

Hizi ni baadhi ya sababu ambazo zinatushurutisha kuhifadhi mnazi.

Tusinywe mvinyo huu kiholela ili kuzuia ndoa zetu dhidi ya kudidimia.