Vyombo vya usalama vinapaswa kuchukua tahadhari za mapema pamoja na kuweka mikakati ya kukabiliana na ghasia zinazoshuhudiwa katika mikutano ya kisiasa.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Hivi majuzi, mkutano wa kuadhimisha siku ya Mashujaa katika uwanja wa Tononoka ulikatizwa kwa muda, baada ya makundi hasimu yaliyogawanyika kwa msingi wa kisiasa kulumbana na kuzua vurugu katika mkutano huo.

Siku ya Jumapili, Ababu Namwamba, mkuu wa chama cha Labour alivamiwa na genge la vijana alipokuwa akitoka katika kanisa moja huko Bangladesh, eneo bunge la Jomvu.

Vijana hao waliuzuia msafara wa Ababu huku wengine wakiwa wamejihami kwa vifaa kama nyundo.

Visa hivi viwili vinaweza kutumika kama onyo kwa wakuu wa usalama kuhusiana na taswira ya uchaguzi mkuu ujao.

Wanasiasa wanaodaiwa kufadhili magenge ya wahalifu wanafaa kukabiliwa kisheria kama njia moja wapo ya kuzima cheche hizi kabla hazijakomaa na kuwa moto utakaoweza kuangamiza hatua za maendeleo ambazo tayari tumezipiga.

Nijambo la kusikitisha kuwaona kina mama ambao ni walezi wakiungana na kuzua ghasia katika mikutano.

Picha waliyotuma kwa watoto wanaolea sio nzuri kwa kuwa yanahujumu maadili na tamaduni zetu.

Mbali na vyombo vya usalama kuwajibika, jamii pia inapaswa kufahamu umuhimu wa amani.

Tusiuze amani kwa hela wanasiasa wanazotupa kwani hatuwezi nunua amani.