Hofu imezuka katika eneo la Kiganjo, Thika katika Kaunti ya Kiambu Jumamosi jioni baada ya jengo moja kuporomoka na kuwaangukia watoto waliokuwa wakicheza ndani ya jengo hilo.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Mmiliki wa jengo hilo la kusukia nywele ambaye hakuwa amefungua kazi siku hiyo na kwa vile jengo hilo halina mlango wa kufunga, watoto waliona mahala pazuri pa kuchezea bila kujua hatari iliyokuwa imewakodolea macho.

Wakaazi wa eneo hilo waliokuwa wakiendelea na shughuli zao za kila siku waligutushwa na poromoko hilo pamoja na kelele za watoto hao na kujaribu kuwaokoa watoto hao waliokuwa wamefunikiwa na jengo hilo.

Japokuwa wakaazi hao walifanikiwa kuwanusuru watoto hao sita, wengi wao walikuwa na majeraha makubwa ya kukatwa na mabati ya jengo hilo huku wengine wakiwa wamevunjika miguu na mikono.

“Nlikuwa dukani mwangu nikiwahudumia wateja wangu ndipo nikasikia kelele upande wa nje ambapo niliona watu wakikimbia kuelekea ‘Salon’ iliyokuwa imeporomoka ndipo nkakumbuka kuwa pia mtoto wangu alikuwa akicheza mle ndani lakini habaari njema ni kuwa wasamaria wema walifika kwa wakati ufaao na kuwaokoa watoto hao,” alisema Mama wangari, mfanyibiashara katika eneo hilo.

Punde tu nimetoka kazini nikija kuingia nyumbani mwangu niliskia kelele nje na kufika niliwapata watoto wamefunikwa na jengo hilo ambapo mimi na watu wengine tulifanya hima kuwatoa upande wa nje pale wengi wao walikuwa wakivuja damu nyingi kutokana na majeraha ya mabati,” alisema Susan Munee mkaazi wa eneo hilo.

Kisa hicho kiliwatia hofu wakaaji hao kwani jengo hilo limekuwa hapo kwa muda mrefu sasa na watoto wao walichezea mle iwapo mwenyewe hajafungua.

Manusura walipelekwa katika Hospitali ya Thika Level Five huku mwenye jengo hilo akibaki kuwasuka wateja wake nje.