Idara ya Jeshi jijini Mombasa imetoa viti magurudumu kwa wanafunzi wanoishi na ulemavu katika Shule ya msingi ya Mtongwe.
Wanajeshi hao walisema kuwa hatua hiyo ni njia moja wapo ya kuwakumbuka wenzao waliopoteza maisha yao wakiwa kazini wakilinda taifa.
Haya yanajiri huku kikosi hicho kikikaribia kuaadhimisha siku ya KDF ambayo hufanyika tarehe Oktoba 14, kila mwaka.
Akihutubia wanahabari, mkuu wa kambi la jeshi la wanamaji kambi ya Mtongwe, Bregedia Lonena Naisho alisema idara hiyo iko imara kukabiliana na magaidi nchini.
Wanajeshi hao pia waliungana na wakaazi katika zoezi la kuchangisha damu.
“Pia tumeweza kutoa damu ambayo itatumika kutusaidia katika siku za usoni kwani tukiwa vitani wanajeshi hupoteza damu nyingi,” alisema Naisho.