Mahakama kuu imeagiza kuondolewa kwa jina la mratibu mkuu wa ukanda wa Pwani Nelson Marwa kwenye kesi ya kumuharibia jina mwanabiashara Arub Katri.
Mahakama kuu ya Mombasa imemuagiza mlalamishi Katri kuishtaki afisi ya mkuuwa sheria badala ya Marwa binafsi.
Jaji Njoki amesema kuwa Marwa hafai kushtakiwa kibinafsi ikizingatiwa alisema maneno hayo akiwa kazini kwa mujibu wa katiba.
“Alikuwa kazini kwa mujibu wa sheria, hivyo hawezi kushtakiwa kibinafsi bali afisi ya mkuu wa sheria ndio inastahili kushtakiwa”,alisema Njoki.
Ikumbukwe mwezi Januari mwaka huu, Marwa anadaiwa kutoa matamshi ya kumuharibia jina mwanabiashara huyo, siku chache baada ya kutiwa mbaroni.