Gavana Kinuthia Mbugua amewauliza wakaazi wa kaunti ya Nakuru kujitokeza kwa wingi kwenye uwanja wa afraha tarehe 16 April. 

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Hii inafuata baada ya Rais Kenyatta kutoa habari kua uwanja huo utatumiwa kwa sherehe za shukrani kufuatia kuachiliwa huru kwa Ruto na Sang na mahakama ya kitaifa ya ICC. 

"Nawauliza wakaazi wa Nakuru kujitokeza kwa wingi afraha tarehe kumi na sita mwezi huu tumpokee rais na naibu wake," alisema Mbugua.

Mbugua alikua akiwahutubia wananchi wa kaunti ndogo ya bahati. Mbugua amezuru bahati kwenye programu ya gavana mtaani inayoendelea katika kaunti zote ndogo 11 za Nakuru.