Akizungumza katika shule ya upili ya Kisii, waziri wa elimu Fred Matiangi aliwaonya walimu wanao jishughulisha na maswala ya siasa kuwa ni heri wajiuzulu na kuingia katika siasa.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Waziri Matiangi alikuwa akizungumza na Walimu wakuu waliokuwa wamekongamana huko, akiwaonya wale wanao azimia kuingia katika siasa ilhali wanaendelea kushikilia nyadhifa za uongozi kukoma kufanya hivyo.

“Nina majina ya walimu wanao azimia kuingia katika siasa mwaka ujao, tuna walimu wa kutosha watakao chukua nafasi zenu mtakapo toka,” alisema Matiang'i.

Matiangi Alisema kuwa ametambua kwamba baadhi ya walimu ni wakurugenzi katika Shirika la maendeleo ya ustawi majani (Kenya Tea Development Agency, KTDA) na kuwaonya kuwa ni lazima walimu wawe shuleni wakati wote ili matokeo yawanafunzi yaboreke.

Matiangi aliwanyoshea kidole cha lawama wadhamini wanaoingilia maswala ya shule na viongozi na kutatiza elimu ya wanafunzi. Alisema kuwa sheria za wizara ya elimu haiwapi wadhamini uwezo wa kuhamisha walimu wakuu wa shule.

Alipongeza shule kama St Charles Lwanga na shule ya wasichana ya Ichuli kwa kuhakikisha kila mwanafunzi anatumia kitabu chake mwenyewe.