Gavana wa Mombasa Hassan Joho akiwahutubia wafuasi wake katika hafla ya awali. [Photo/ nairobiwire.com]

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Gavana wa Mombasa Hassan Joho ameikosoa hotuba ya Rais Uhuru Kenyatta ya sherehe za Madaraka, na kuitaja kama iliyojaa siasa za kujipigia debe.

Akizungumza siku ya Alhamisi katika uwanja wa Tononoka wakati wa sherehe hizo za Madaraka, Joho alisema kuwa hotuba hiyo haikuangazia mahitaji muhimu ya mwananchi wa kawaida.Joho aliukosoa mradi wa kusambaza umeme kwa kusema kuwa sehemu kubwa ya nchi haina umeme kinyume na inavyosema Jubilee.“Sehemu nyingi hazina umeme kama vile Jubilee inavyojipigia debe kuhusu swala hilo,” alisema Joho.Aidha, gavana huyo alisema kuwa vituo vingi vya kupiga kura havina umeme bali vinatumia koroboi.“Vituo vingi vya kupigia kura na kukagua kura huwa havina umeme. Sasa nashindwa huu umeme wa Jubilee umewekwa wapi?” aliuliza Joho.Hata hivyo, mwaniaji wa useneta Mombasa kupitia chama cha Jubilee Abdulsallam Kassim amemkosoa Joho kwa kupinga hotuba ya rais.“Hotuba ya raisi imeangazia mahitaji yote ya mwananchi, Joho hana la kusema ndiposa anajaaribu kupinga hotuba hiyo,” alisema Abdullasam.Aidha, amemtaka Joho kutokashifu vitengo vya usalama na kukoma kuhusisha polisi na mrengo wowote wa kisiasa.Vile vile alipinga madai ya Joho kuwa reli ya kisasa ya SGR itaathiri ajira za wakaazi wa Mombasa na kumtaka gavana huyo kuweka wazi miradi aliyofanya.“Anafaa kuweka wazi miradi ambayo amewafanyia wananchi wa Mombasa badala ya kujisifu ovyo ovyo,” alisema Abdullasam.