Gavana wa Mombasa Hassan Joho amemkosoa mbunge wa Lunga Lunga Khatib Mwashetani kwa kudai kuwa chama cha Ford Kenya kitajiondoa katika mrengo wa Cord iwapo Moses Wetangula hatachaguliwa kama mgombea wa urais.
Akiongea afisini mwake siku ya Alhamisi, Joho amesema kuwa maswala ya nani atakayechaguliwa kupeperusha bendera ya Cord itasuluhishwa wakati wake ukifika na wajumbe wa mrengo huo.
Joho pia amemtaka Mwashetani kuacha kuongea kwa niaba ya chama hicho akisema kuwa ni mtu mdogo sana kufanya uamuzi wowote katika chama hicho.
Hapo awali, Mwashetani alikuwa amesema kuwa chama cha Ford Kenya kitajiondoa katika mrengo wa Cord kwa kuwa wanahisi kuwa hakuna demokrasia katika chama hicho.