Gavana wa kaunti ya Mombasa Ali Hassan Joho amemuandikia barua waziri wa usalama wa ndani Joseph Nkaissery akitaka haki itekendeke kuhusu kupukonywa kwa silaha anazomiliki.
Barua hiyo iliyowasilishwa katika afisi ya waziri Nkaissery na wakili wake Ahmednassir Abdullahi, imesema kuwa agizo hilo linakiuka haki za kiuongozi kwani Gavana Joho anastahili kupewa ulinzi sawa na viongozi wengine.
Joho amesema kuwa japo amesalimisha tayari silaha moja jinsi alivyoaginzwa na afisa mkuu msajili wa silaha nchini Samuel Kimaru, kuna haja ya swala hilo kuangaziwa kwa makini na haki kutendeka.
Joho amesema kuwa Kimaru amechukua agizo la kumpokonya silaha kufuatia vurugu la uchaguzi mdogo wa Malindi uliyofanyika siku ya Jumatatu wiki iliyopita kuwa kiongozi huyo alihusika kuwaagiza walinzi wake kuwanyanyasa wakaazi, madai ambayo Gavana Joho aliyakanusha.
Sasa Joho kupitia wakili wake Ahmednassir anataka serikali kuchunguza swala hilo kwa kina na kuhakikisha kuwa haki dhidi ya gavana huyo inatendeka kwa usawa.