Gavana wa kaunti ya Mombasa amewaacha wengi na vicheko baada ya kumuita aliyekuwa rais wa kwanza wa taifa la Kenya hayati mzee Jomo Kenyatta jina la mtaani lifaamikalo kama buda.
Neno Buda ni jina la kimitaani linalomaanisha baba.
Neno hili hutumiwa sana na vijana hasa wa Pwani wakiwa maskani mwao.
“Rais wa kwanza wa taifa hili ambaye ni buda wa rais wa sasa alikuwa hakosi kuhudhuria sherehe hizi za kilimo kila mwaka katika uwanja huu wa kilimo,” alisema Joho.
Viongozi mbali mbali waliokuwa kwenye maonyesho ya kilimo jijini Mombasa wakiongozwa na rais Kenyatta walipasua vicheko baada ya kusikia jina hilo la utani.
Hatimaye Joho aliomba msamaha kwa kumuita jina hilo aliyekuwa raisi wa kwanza wa taifa hili.
“Samahani kwa kumuita jina hilo marehemu ambaye ni baba wa kwanza wa taifa letu,” alisema Joho.