Gavana wa Mombasa Hassan Joho amepata afueni kwa mara ya pili baada ya Mahakama kuu kumwongezea muda wa kuizuilia serikali kumpokonya bunduki.
Akitoa uamuzi wake siku ya Ijumaa, Jaji George Odunga alisema agizo la serikali kutaka kumpokonya gavana huyo bunduki ni kinyume cha sheria.
Aidha, alisema kuwa Waziri wa usalama wa ndani Joseph Nkaissery alipitiliza majukumu yake.
Hatahivyo, Msajili wa silaha Samuel Kimaru, aliambia mahakama kuu kuwa yuko na jukumu na nguvu za kufutilia mbali kibali cha umiliki wa bunduki za Joho.
Kesi hiyo ilahirishwa baada ya Joho kupitia mawakili wake kusema kuwa hawakuwa tayari kuendelea na kesi hiyo baada ya kutokabidhiwa nakala muhimu za kesi hiyo na mwendesha mashtaka.