Wakaazi wa eneo bunge la Lunga Lunga katika kaunti ya Kwale wametoa onyo kwa Gavana wa Mombasa Hassana Joho wakitaka asiingilie maaswala ya siasa katika eneo bunge hilo.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Wakiongozwa na kiongozi wa wanawake Lucy Ruwa wakaazi hao wamesema kuwa hawatakubali viongozi kutoka nje ya eneo bunge hilo kuwachagulia viongozi katika uchaguzi mkuu wa 2017.

Aidha Ruwa amewakashifu magavana Hassan Joho wa Mombasa na Amason Kingi wa Kilifi kwa kuandaa msururu wa mikutano za kisiasa katika eneo hilo huku wakitoa matamshi za dharau kwa mbunge wa eneo hilo Khatib Mwashetani.

Ni vyema viongozi wetu waheshimiwe licha ya msimamo wowote wa kisiasa ambayo wanachukua na hatutamruhusu mtu yeyote kuja hapa na kumtukana mbunge wetu”Ruwa alisema.

Kiongozi huyo wa wanawake akiandamana na zaidi ya viongozi 20 kutoka kabila mbali mbali katika eneo la lungalunga sasa wanamtaka Joho kubakia katika siasa za kaunti ya Mombasa na kumuonya dhidi bya kuvuka mpaka.