Gavana wa kaunti ya Mombasa Ali Hassan Joho amesisitiza tena azimio lake la wa kuwania kiti cha uraisi mwaka 2022.
Joho alisema siku ya Jumapili katika eneo la Magongo kuwa yuko na matumaini ya kupata kiti hicho iwapo wananchi watajitokeza na kumuunga mkono.
Ameongeza kuwa yuko tayari kubadilisha uongozi alioutaja kuwa wa kibepari unaongozwa na muungano wa Jubilee.
Aidha, aliwataka wanachi wa Mombasa na Pwani kwa jumla kutwaa vitambulisho vitakavyowasaidia kuwa wapiga kura, ilikupitisha uongozi wa Cord madarakani.