Gavana wa Mombasa Hassan Joho ameshikilia msimamo wake wa kukataa walinzi wa serikali.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Akiwahutubia wanahabari mjini Mombasa siku ya Jumanne, Joho alisema kuwa hawezi kuchaguliwa maafisa wanaostahili kumlinda.

Gavana huyo amesisitiza kuwa kuna njama fiche ya idara ya usalama kuhusu walinzi wapya ambao alikuwa amepewa na serikali.

Joho alidai kuwa walinzi hao walikuwa wametumwa kumwekea vitu haramu ndani ya gari lake ama nyumbani kwake, kisha baadaye wamuhusishe navyo.

Alisisitiza hatokubali kuchaguliwa walinzi kwa kuwa katiba inamruhusu kuchagua walinzi anao wataka.

“Hakuna kiongozi yeyeto ambaye alichaguliwa askari, kila mtu yuko na haki ya kuchagua walinzi wake,” alisema Joho.

Ikumbukwe kuwa Joho alipokonywa walinzi wake mwezi Januari baada ya kumkemea Rais Uhuru Kenyatta hadharani jijini Mombasa.