Gavana wa Mombasa ametoa ushahidi wake kwenye kesi ya kupinga ushindi wake. [Photo/The Star]
Joho amekanusha madai kuwa alihusika kuwashurutisha wasimamizi wa uchaguzi dhidi ya kumtangaza yeye kama mshindi wa uchaguzi wa Agosti nane.
Akitoa ushahidi huo siku ya Alhamisi,mbele ya jaji Lydia Achode,alisema kuwa yeye ndie mshindi halali kwa mujibu wa tume ya uchaguzi nchini Iebc,hivyo basi hakuna wizi wa kura aliofanya.
“Mimi ndion mshindi halali nliyechaguliwa,hakukuwa na wizi wa kura kabsa,wapigakura walinichagua kwa upendo wao”,alisema Joho.
Aidha,alisema kuwa aliweza kuwashinda wapinzani wake kwa kura nyingi hivyo basi akabuka mshindi mwenye kura nyingi.
“Wapinzani wangu niliwashinda kwa kura nyingi sasa wanadai kuwa kulikuwa na wizi wa kura,huo ni urongo”,asema Joho.
Ikumbukwe tayari Aliyekuwa Seneta wa Mombasa Hassan Omar alitoa ushahidi wake katika kesi ya kupinga ushindi wa Gavana wa Mombasa Hassan Joho katika mahakama kuu ya Mombasa mwezi uliopita.
Omar alisema kuwa kulikuwa na udanganyifu mwingi wa kura katika vituo mbali mbali Kaunti ya Mombasa.
Akitoa ushahidi wake mbele ya Jaji Lydia Achode, Omar alisema kuwa kuna wapiga kura waliokuwa wanapewa zaidi ya makaratasi mawili ya kupigia kura katika eneo bunge la Changamwe.
“Kuna wapiga kura waliopewa zaidi ya makaratasi mawili ya kupigia kura katika eneo la Changamwe. Huu ni wizi wa kura,” alisema Omar.
Aidha, Omar alisema kuwa wapiga kura wengi walifurushwa baada ya majina yao kukosekana kwenye vifaa vya Kiems.
“Wapiga kura walifurushwa katika vituo vya kura baada ya majina yao kukosekana kwenye kifaa cha Kiems, hatua ambayo ni ukiukaji wa haki za wapiga kura,” alisema Omar.
Omar ameitaka mahakama kutupilia mbali ushindi wa Joho na uchaguzi huo kufanyika upya.
Kesi ya kupinga ushindi wa Joho iliwasilishwa mahakamani na Omar baada ya Joho kupata ushindi wa kura 221,177 huku Omar akijizolea kura 43,287.