Wabunge kadhaa kutoka kaunti ya Mombasa wamesifu hatua ya Gavana Hassan joho kutangaza kuwania kiti cha urais mwaka wa 2022.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Viongozi hao wamesema kuwa wako tayari kumuunga mkono kwa vyovyote vile.

Wakihutubia mkutano wa hadhara Magongo, Mbunge wa Mvita Abduswamad Sherrif, Mbunge wa Kisauni Rashid Bedzimba, mbungwe wa Changamwe Omar Mwinyi, mbunge wa Jomvu Twalib Badi na mwakilishi wa wanawake Mishi Mboko walisema kuwa umefika wakati wa viongozi kutoka Pwani kuiongoza nchi.

“Tumewaunga mkono viongozi kutoka sehemu zingine za nchi kwa miaka mingi na ifikapo mwaka wa 2022 hata nasi tunatoa wito watuunge mkono,” alisema Abduswamad.

Aidha Gavana Joho alisema kuwa ni vibaya viongozi kutuka eneo mbili nchini kuwa watawale nchi daima akisema kuwa kuna sehemu zingine pia zaweza kutoa rais.