Gavana wa kaunti ya Mombasa Ali Hassan Joho amewataka wakazi wa Likoni kumpigia kura kwa hatamu ya mwisho ifikapo uchaguzi mkuu 2017.

Share news tips with us here at Hivisasa

Akizungumza mnamo siku ya Jumapili katika uwanja wa shule ya Msingi ya Catholic, gavana Joho amewaomba wakazi kuunga mkono azma yake ya kuwania ugavana tena chini ya mrengo wa Cord na kuwaahidi miradi na maendeleo mengi kabla ya uchaguzi mkuu. 

Gavana huyo wa Mombasa alikuwa amehudhuria hafla ya uzinduzi wa mradi wa maji wa kundi la vijana la kujitegemea la kedeo la Likoni. 

"Naomba kura zenu kwa wingi ndiposa tuweze kushinda. Hii itakuwa mara ya mwisho kwangu mie kuwania ugavana. Mwaka wa 2022 nitawania Urais wa nchi ya Kenya," alisema. 

Gavana Joho alikuwa ameandamana na wawakilishi wadi wa Mombasa na mwakilishi wa wanawake Mishi Mboko ambaye amejitosa kwenye kinyang'anyiro cha kiti cha ubunge eneo la Likoni.